Jumanne, 29 Desemba 2015

MAJI NI UHAI!!, MAJI NI KIFO.

Katika maisha ni vigumu kukua bila kusikia ili neno, “maji ni uhai”  katika hali halisi ya dhana maji ni uhai tunaambiwa maji uchukua asilimia kubwa ya mwili wa binadamu pia maji kwa kiasi kikubwa ndio yamezunguka uso wa dunia.

mkufunzi wa uogeleaji akiwa na wanafunzi katika mazoezi
Maji ni uhai kwa kuwa mwili wa binadamu una uhuitaji wa maji pia viumbe hai vyote kwa kiasi kikubwa utegemea maji ili viishi. Lakini maji pia ni chanzo cha kupotea kwa uhai kwa viumbe hawa ambao utegemea sana maji.

Dunia imeshuhudia vifo vingi vya maji inapotekea majanga kama kuzama kwa meli, mashua na boti, lakini pia inapotokea mafuriko. Majanga haya ugharimu maisha ya watu wengi zaidi. Lakini pia uzembe wa kutofunika baadhi ya mashimo hama vyombo vya maji navyo vimekuwa vikigharimu uhai.

Kumekuwa na matukio mengi ya watu kudumbukia kwenye madibwi na kupoteza maisha ila pia watoto majumbani kufariki kwa kudumbukia kwenye vyombo vyenye maji ama visima.
Kama maji ni uhai je kwa nini vifo hivi vinatokea? Jibu la swali hili linaweza kuwa gumu kidogo lakini kwa jibu la kawaida ni kuwa kila chenye uzuri hakikosi ubaya au wengine wanasema ukizidisha kilakitu kinakuwa sumu.

Maana yake ni kuwa maji yasipotumiwa vizuri yaani kuchukua tahadhari na kujua hatari za maji bhasi ni chanzo kikubwa cha kupotea kwa maisha.
boya la kuokolea
Je vifo vya maji ni mpango wa Mungu?
Stewart Kiluswa mkufunzi wa uogeleaji kwa kujiokoa na kuokoa maisha, anasema, vifo vingi vya maji hutokea kutokana na uzembe na kutokujua hatari za maeneo watu wanamoishi au jinsi ya kujioka na hatari za maji.

Unawezaje  kutambua hatari za maji na jinsi gani ya kujikinga nazo.
Kujua hatari za maji ni vyema kuwa na mwenyeji au kuuliza wenyeji  hali halisi ya mazingira ya maji uliopo, kama kuna wanyama wakali, mikond mkali wa bahari au kama kuna alama kataza (zinazozuia) matumizi ya eneo hilo. Pia kuwa waangalifu na vyombo vya maji kama ndoo na baseni hasa hasa tunapokuwa na watoto wadogo, pia kuhakikisha mazingira yetu yenye mashimo makubwa yanawekea alama za tahadhari ili kuzuia majanga. Mara nyingi watoto upenda kwenda kucheza wakiwa peke yao ni vyema kujua wanachezea maeneo gani na kama ni eneo la maji ni vyema wakawa na uangalizi wa mkubwa.
mmoja wa wanaojifinza kuogelea

Jinsi  ya kujiokoa na kuokoa mtu aliye katika hatari ya kufa maji.
Kuna aina ya watu wane wanaokuwa katika hatari ya kufa maji nao ni:
Asiyejua kuogelea kabisa, anayejua kuogelea kidogo, anayejua kuogelea  na aliyepoteza fahamu majini

Asiyejua kuogelea  huyu mara nyingi akiwa katika hatari ya kufa maji huzama na kuibuka akiwa katika hali ya wima, ilihali anayejua kuogelea kidogo huzama na kuibuka akiwa katika hali ya mshazali na mara nyingi hujitahidi kuelekea sehemu ambayo anaweza kupata musaada kwa haraka, huyu ujitahidi kujaribu kuogelea ndio maana huwa  katika hali ya mshazali.

Anayejua kuogelea, anaweza kuwa katika hatari ya kufa maji kutokana na sababu kama kushambuliwa na wanyama au wadudu wa majini na hvyo akili yake yote uhiamishia palipo na jeraha ila pia anaweza kuwa amebanwa na matatizo ya msuli hivyo vyote vinaweza kupelekea maisha ya mtu kuwa hatarini kwenye maji.

Aliyepoteza fahamu huyu ni kwamba anakuwa ajitambui na mwili wake unaweza kuwa unaelea au umezama chini.

Wakati wa kuwapatia msaada wa uokozi jitahidi sana kutokumgusa mtu ambaye bado ni mzima yaani ajapoteza fahamu. Tumia nyenzo yoyote ile ambayo ataweza kuishika na ww kumvuta kwa kutumia hyo nyenzo, mfano wa nyezo za  uokozi ni kama maboya, mti mrefu, kamba au kidumu chenye mfuniko kilichofugwa kamba au nguo au kitu chochote kinachoelea, kumbuka wakati unajaribu kuokoa hakikisha maisha yako ni salama. Kwa mtu ambaye amepoteza fahamu unaweza kumfikia na kumshika wakati wa kumtoa kuelekea nchi kavu.


Maji ni uhai ila pia maji ni chanzo cha vifo, tujihadhari katika matumizi ya maji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni