Jumanne, 30 Juni 2015

MILLEN MAGESE, EDDY KENZO WAIBEBA EAST AFRICA TUZO ZA BET

tuzo aliotunukiwa Millen
Mwanamitindo na Mrembo wa Tanzania mwaka 2001, Happiness Millen Magese ametunukiwa tuzo ya pekee ya BET mwaka huu iitwayo ‘Global Good Award’
Millen amepewa tuzo hii kutokana na jitihada zake za kampeni ya ugonjwa wa endometriosis (ugonjwa unaosababishwa na seli za tumbo la uzazi kuwa nje ya kizazi) ambao amekuwa nao katika maisha yake yote tangu awe msichana.

Millen ameanzisha taasisi ya kuwasaidia wanawake wengine  hapa nchini ya Millen Magese Faundation ili waepuke kile ambacho kilimkuta yeye. Pamoja na hivyo Millen amekuwa mstari wa mbele kutoa misaada mbalimbali kwa wasiojiweza.

Eddy Kenzo kwenye red carpet akiwa na wapambe
Katika tuzo hizo pia msaani wa Uganda Eddy Kenzo amebeba tuzo ya msanii bora mpya wa kimataifa anayependwa na watazamaji (Viewer’s Choice Best New International Artist, 2015)
Kaitka kipengele hicho Eddy Kenzo alikuwa akichuana na Assper Nyovest wa Afrika kusini, Mz Vee wa Ghana na wasanii wa uingereza, George the poet, MIC Lowry Na Novelist

Kenzo katika ukurasa wake wa facebook amewashukru washabiki wake, huku akisema ilikuwa ni safari ndefu na akasema ni tuzo ya pekee kwa ukanda wa Afrika Mashariki.


Jumapili, 21 Juni 2015

KIBARUA CHA KOCHA NOOIJ CHAOTA NYASI TAIFA STARS

 kocha  wa stars aliyefungashiwa virago, Mart Nooij
Kibarua cha mholanzi Mart Nooij kimefikia tamati baada ya kikao cha  kamati ya utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kulichokaa  kujadili mwenendo wa timu ya taifa, Taifa Stars. Mkataba wa Nooij na Taifa Stars ulikuwa umebakia miezi 10

Pia Kamati hiyo imevunja  benchi la ufundi la timu hiyo mpaka benchi jipya litakapotangazwa.

Kibarua cha Nooij kinafikia tamati baada ya kufuingwa mechi tano mfululizo zikiwemo mechi kati ya Lesotho, Madagascar, Botswana, Misri na mechi ya jana dhidi ya Uganda ambayo Stars imeambulia kipigo cha mabao 3-0 katika uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Tangu Nooij aichukue stars April mwaka jana Kutoka kwa Kim Poulsen, ameiongoza timu hiyo katika mechi 18 kati ya hizo ameshinda mechi 3, sare mechi 6, na kufungwa mechi 9



Jumamosi, 20 Juni 2015

KWA MATOKEO HAYA,JE SAFARI YA NOOIJ IMEWADIA?

Erisa Sakimbu mfungaji wa mabao mawili ya The Cranes(picha kutoka Bin Zubery)
MABAO mawili ya mshambuliaji Erisa Sekisambu  wa timu ya taifa ya uganda, the cranes,yanaweza kuwa yamehitimisha historia ya kocha Mholanzi, Mart Nooij katika timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars baada ya kufungwa 3-0 na Uganda usiku huu katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar. 

Mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza kufuzu michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) itakayofanyika Rwanda mwaka 2016, Sekisambu alimtungua kipa Deo Munishi ‘Dida’ bao moja kila kipindi, wakati bao la tatu lilifungwa na Farouk Miya dakika ya 89.

Mechi hiyo ni ya tano mfululizo Stars kufungwa, baada ya awali kufungwa na Madagascar, Lesotho, Botswana katika michuono ya COSAFA ambayo stars ilishiriki kama mwalikwa, na wiki iliyopita ikaambulia kipigo kutoka kwa misri.

Jumatano, 17 Juni 2015

LIGI KUU UINGEREZA KUTIMUA VUMBI AGOSTI 8

Mabingwa watetezi Chelsea the Blues wataanza kutetea taji lao la ligi kuu katika uwanja wao wa nyumbani wa Stamford Bridge watakapo pambana na Sweswea  katika mechi za ufunguzi zitakazopigwa kati ya Agosti 8-9.

Washindi wa pili Man city wao watasafiri kwenda kuwakabili west bromwich albion, huku majirani zao Machester United wakiwakaribisha Tottenham Old Trafford.

Mabingwa wa kombe la FA Arsenal wao watakuwa nyumbani kuwakaribisha wagonga nyundo wa jiji la London, huku majogoo wa anfield timu ya liverpool watasafiri kwenda kuwakabili

Ijumaa, 12 Juni 2015

LAPTOP ZILIZOTENGENEZWA KENYA

Chuo Kikuu cha Kilimo na technologia cha Jomo Kenyatta Nchini Kenya, JKUAT, leo kimezindua kumputa mpakato iliyotengezwa nchini humo.

JKUAT kwa kushirikaina na wizara ya Viwanda Na Ujasiriamali imezindua laptop hiyo yenye ukubwa wa Corei3, 4GB na 500GB kwa habari zaidi tembelea tuko.co.ke

Dr. Mauki: PATA KUJUA VITU VINGI ILI UWE NA MAMLAKA

                                     Dr.Mauki akiwa na baadhi ya wanafunzi baada ya Mhadhara

Mwalimu na mtaalam wa maswala ya mahusiano Dr.Chris Mauki ametoa rai kwa vijana kujifunza mambo mengi yenye maana na yanayoendana na malengo yao ili waweze kuwa na mamlaka kwa yale wanayoyatenda.

Akizungumza kwenye Mhadhara  katika chuo kikuu cha Tumaini Dar es Salaam. Dr. Mauki amesema kuna njia tano ambazo mtu anaweza kuzitumia kufikia mafanikio na kuwa na mamlaka.

Njia hizo amezitaja kuwa ni pamoja na kutengeneza mtaji wa watu (social capital), kutambua vipawa na talanta ndani ya mtu na kuziendeleza(discover the talent within You), kutimiza majukumu na kuacha uvivu(be responsible and dont be lazy), kuacha kupoteza muda ukitafuta kazi  badala yake kutumia muda kutatua matatizo kwenye jamii(use time effectively to solve problem), na kuepuka wanaokudharau na kuwakumbatia wanaokutia moyo na kukukosoa kwa moyo wa upendo(dont let any discouragement on you, associate yourself with positive critics people).
"huwezi kuwa na mamlaka juu ya jambo kama ujui vitu vingi kuhusu hilo jambo, kipaji pekee akitoshi juhudi inahitajika kuhakikisha unakuwa na mamlaka kwenye kitu ambacho wewe ni bora".

Dr. mauki amesema si jambo la busara kupoteza muda kutaka kutenda bila kuweka juhudi kwenye vitendo, huku akisisitiza wengi wa waliofanikiwa ni watu ambao wamekuwa na macho ya mwewe wakijaribu kuona mbali. kwa kutumia vipawa walivyonavyo.