Taasisi ya maendeleo ya Mpira wa Kikapu🏀 inayomilikiwa na Kocha wa klabu ya San Fransisco kwa kushirikiana Jamtown Gym na wadau wengine wa Marekani wamekubali kushirikiana na Chama cha mpira wa Kikapu nchini (TBF) kuendeleza mchezo huo nchini.
Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya Rais wa TBF Phares Magesa kufanya ziara ya Kikazi nchini humo na kukutana na Kocha wa San Fransisco, Ameer Aziz ambaye wamekbaliana kuendesha mafunzo kwa vijana wadogo.
"miongoni mwa tuliyokubaliana ni kuendesha mafunzo kwa vijana wadogo , mafunzo hayo yatafanyika Tanzania na pia Marekani ambapo baadhi ya vijana watapatiwa nafasi za kufanya mafunzo Marekani na pia vijana wa Marekani watatembelea Tanzania kufanya mafunzo na vijana wetu, timu yetu ya Taifa ya Vijana itapatiwa nafasi ya kujifunza zaidi Marekani na kupewa michezo ya majaribio na timu nyingine za mataifa mengine ambazo nazo zitaalikwa kutoka mabara mengine katika mashidano maalumu, kutoka Afrika ni Tanzania pekee ndio tumepewa nafasi hiyo" Alisema Magesa.
Ameongeza kuwa Taasisi hiyo itakuwa inasaidia kuratibu upatikanaji wa vifaa vya michezo Marekani na kuvileta Tanzania, pamoja na kutafuta wafadhili watakaoweza kusaidia utekelezaji wa programs za maendeleo ya kikapu ili kukuza mchezo huu nchini.
Mbalo na hayo ushirikiano huo pia utashuhudia wachezaji kadhaa nyota wa kikapu duniani wakitua nchini kuendesha Clinics za kikapu.
Ameongeza kuwa Tanzania itafaidika na kuratibu mradi wa ujenzi wa viwanja vya kikapu nchini, kutoa nafasi ya mafunzo kwa Timu zetu zote za Taifa kufanya mafunzo maalumu katika Gym ya Jamtown iliyoko Oakland, California.
"Timu zetu zitapata nafasi kutumia Gym bora kuliko zote hapa Marekani na inatumiwa pia na wachezaji wengi mahiri kwa mazoezi binafsi wakiwemo Stephen Curry na Kelvin Durant,Taasisi hii pia itaratibu na kujenga ushirikiano kati ya timu za Tanzania na baadhi ya timu mahiri za NBA ikiwemo timu ya Golden State Warriors".Aliongeza Magesa.
Aidha amewataka wadau nchini kushirikiana na TBF katika maendeleo ya Mchezo wa Kikapu.
TBF ipo kwenye maandalizi ya kuandaa michuano ya Kanda ya Tano kwa vijana wenye umri chini ya miaka 18 (FIBA Zone V U18) itakayofanyika June 2018 jijini Dar es Salaam.
🏀






