Jumamosi, 11 Julai 2015

MMOJA ASHIKILIWA NA POLISI KUELEKEA MKUTANO MKUU CCM

Polisi Dodoma inamshikilia mtu mmoja mwenye asilia ya Asia akiwa na kiasi kikubwa cha fedha, ahusishwa na mchakato wa mchujo unaondelea.
Raia anaedaiwa kukamatwa, pamoja na fedha alizokutwa nazo

katika mitandao ya kijamii picha za mtu huyo zimesambaa sana huku akihusishwa na mmoja wa wagombea walio katika tano bora, Bernard Membe.

Akielezea sintofahamu hiyo, Bernard Membe ameandika katika ukurasa wake wa twitter akisema, "Kuna taarifa za uongo zinazoenezwa kwamba kuna "Mtu wa Membe" amekamatwa na pesa Dodoma,siasa hizi ni za hovyo kwani hazitajenga Taifa letu. Naomba msihadaike na watu wanaotaka kututia doa baada ya kukosa uchafu dhidi yetu"

LOWASA AKATWA TANO BORA CCM

hatimaye kitendawili cha nani yumo nani kakatwa kimeteguliwa, huku waziri mkuu wa zamani ambaye alijizolea wadhamini wengi, Edward Lowasa akiwa amewekwa pembeni.

Tano bora iliyopitishwa na kamati kuu ya CCM ni Bernard Membe, Dr. John Magufuli, Asha Rose Migiro, January Makamba na Amina Salum Alli.

Baada ya vikao vya kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi (CC) kukaa kwa muda mrefu bila ufumbuzi wa tano bora, huku nchi nzima ikielekeza macho yao mjini Dodoma ambapo vikao hivyo ndo vinafanyika.

katibu uenezi wa chama hicho Nape Nauye amesema majina hayo yatapelekwa halimashauri kuu taifa ambayo ndio itatoa tatu bora kabla ya mkutano mkuu hapo baadae leo hii.



Jumanne, 7 Julai 2015

MBUNGE CHADEMA ANUSURIKA, AJALI YA HELIKOPITA

helikopita baada ya kuanguka.
Mbunge wa Arumeru Mashariki,mkoani Arusha Joshua Nassari amepata ajali ya helkopta aliyokua anaitumia kufanya ziara katika jimbo lake.

Habari za awali tulizozipata ni kwamba mbunge huyo wa Chadema Joshua Nassari amenusurika kufa baada ya Helkopta aliyokuwa anaitumia kuanguka baada ya kunasa kwenye mti baada ya kupotea kwenye mawingu.


Aidha taarifa hizo zinaeleza kuwa Mbunge huyo kwa Tiketi ya Chadema, na rubani wake walitoka wakiwa wazima na wapo katika Hospitali ya Kanisa la Kilutheri ya Selian ya jijini Arusha. 
Mbunge wa Arumeru mashariki, Joshua Nassari akiwa na helicopita aliyopata nayo ajali

Jumamosi, 4 Julai 2015

BUNGENI HAKUKALIKI WANGINE WAPINGWA STOP

Kwa siku tatu mfululizo bunge limekuwa na mzozo ambao umekuwa ukipelekea kuahirishwa kwa vikao vya bunge huku, baadhi ya wabunge wakisimamishwa kuhudhuria vikao vilivyobaki vya bunge hilo ambalo linakoma July 8.

Alhamisi July 02 2015 Mbunge John Mnyika aliomba mwongozo kuomba Bunge lisiendelee kwa vile ishu ya kujadili Miswada mitatu iliyowasilishwa kwa hati ya dharura kwa siku moja ilikuwa inakiuka Kanuni za Bunge, ukatokea mvutano na baadae Spika Anne Makinda akaahirisha Bunge.

Ijumaa July 03 2015 hali ikawa hivyo hivyo tena, wakati Waziri George Simbachawene anasoma Muswada, ikatokea mvutano mwingine, zikaanzishwa kelele Bunge likaahirisha tena.. Kikao cha Jioni Spika Anne Makinda akarudi na list ya majina ya Wabunge ambao wamesimamishwa Bungeni kutokanana maamuzi ya Kamati ya Maadili ya Bunge. 

Leo July 04 2015 Kikao kimeanza tena saa tatu asubuhi, Mbunge Ezekiel Wenjeakaomba Spika atoe ufafanuzi wa kwanini Mbunge Silinde hayuko kwenye list ya waliotajwa kusimamishwa lakini Askari wa Bunge wamemzuia asiingie kwenye Kikao?

Majibu ya Spika hayakuwaridhisha baadhi ya Wabunge, zikaanza tena kelele… Spika akataja list ya Wabunge wengine ambao wanasimamishwa kuhudhuria Vikao vya Bunge kwasiku tano kila mmoja.

Ezekiel Wenje, Mussa Kombo, Masoud Abdallah Salim, Rebecca Ngodo, Sabrina Sungura,Khatib Said Haji, Dr. Anthony Mbassa, Maulidah Anna Valerian Komu, Kulikoyela Kahigi, Cecilia Pareso, Joyce Mukya, Mariam Msabaha, Grace Kiwelu, Israel Natse, Mustapha Akonaay, Konchesta Rwamlaza, Suleiman Bungura, Rashid Ali Abdallah,Ali Hamad,Riziki Juma,Rukia Kassim Ahmed,Azza Hamad,Khatibu Said Haji,Kombo Khamis Kombo,Ali Khamis Seif,Haroub Mohammed Shamisi,Kuruthum Jumanne,Mchuchuli,Amina Mwidau,Mkiwa Kimwanga,Salum Baruhani,Marry Stellah Malaki,Rashid Ally Omary,Mwanamrisho Abama na Lucy Owenya

Jumatano, 1 Julai 2015

RATIBA YA CECAFA KAGAME CUP

Michuano ya kombe la kagame Cecafa kuanza kutimua vumbi Julai 18 hadi Agosti 2 jijini Dar es Salaam, huku wawakilishi wa Tanzania, Timu ya Yanga ilimepangwa kundi A  na Azam ikiwa imepangwa kwenye kundi C.

Mechi ya ufunguzi tarehe 18 Julai, 2015 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam itashuhudia wenyeji Yanga SC wakicheza na Gor Mahia ya Kenya, huku APR ya Rwanda ikicheza na Al Shandy ya Sudan na KMKM ya Zanzibar wakifungua dimba na Telecom ya Somalia.

Timu tatu zitakazoshika nafasi ya juu kutoka kundi A, timu mbili za juu kutoka kundi B & C, na mshindi mwenye wastani mzuri kutoka kundi B & C zitaingia katika hatua ya robo fainali.

KUNDI A
YANGA (Tanzania)
GOR MAHIA (Kenya)
KHARTOUM (Sudan)
TELECOM (Djibout)
KMKM (Zanzibar)


KUNDI B
APR (Rwanda)
AL SHANDY (Sudan)
LLB (Burundi)
ELMAN (Somalia)

KUNDI C
AZAM(Tanzania)
MALAKIA(South Sudan)
KCC(Uganda)
ADAMA City (Ethiopia)

LIGI DARAJA LA KWANZA KUANZA KUTIMUA VUMBI SEPTEMBA 12

Ligi Daraja la Kwanza (FDL)  kwa msimu wa 2015/2016 kuanza kutimua vumbi Septemba 12 mwaka huu.
Ligi hiyo itachezwa katika makundi matatu ya timu nane nane kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

Mfuko huo wa makundi matatu umetokana na marekebisho ya Kanuni za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) yaliyofanywa hivi karibuni na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) 

Mshindi wa kwanza wa kila kundi atapanda kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kwa msimu wa 2016/2017 wakati timu itakayoshika nafasi ya mwisho katika kila kundi itashuka kucheza Ligi Daraja la Pili (SDL) kwa msimu wa 2016/2017.

Kundi A linaundwa na timu za African Lyon FC (Dar es Salaam), Ashanti United SC (Dar es Salaam), Friends Rangers FC (Dar es Salaam), Kiluvya United FC (Pwani), Kinondoni Municipal Council FC (Dar es Salaam), Mji Mkuu FC (Dodoma), Polisi Dar es Salaam na Polisi Dodoma.

Timu zinazounda kundi B ni Burkina Faso FC (Morogoro), Kimondo SC (Mbeya), Kurugenzi Mafinga FC (Iringa), Lipuli FC (Iringa), Njombe Mji FC (Njombe), Polisi Morogoro na Ruvu Shooting (Pwani).

Kundi C ni Geita Gold SC (Geita), JKT Kanembwa FC (Kigoma), JKT Oljoro (Arusha), Mbao FC (Mwanza), Panone FC (Kilimanjaro), Polisi Mara, Polisi Tabora na Rhino Rangers (Tabora).

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO


Jumla ya wanafunzi 55,003 wakiwemo wasichana 23,303 na wavulana 31,700 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2015

Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali. Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 29,744 wakiwemo wasichana 11,450 na wavulana 18,294 sawa na asilimia 54.08 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati; na wanafunzi 25,259 wakiwemo wasichana 11,853 na wavulana 13,406 sawa na asilimia 45.92 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2015 wataanza muhula wa kwanza tarehe 18 Julai, 2015, hiyo ni kwa mujibu wa  Ofisi ya Waziri Mkuu-Tamisemi.



Bonyeza hapa kupata orodha ya wanafunzi waliochaguliwa