![]() |
| Erisa Sakimbu mfungaji wa mabao mawili ya The Cranes(picha kutoka Bin Zubery) |
MABAO mawili ya mshambuliaji Erisa Sekisambu wa timu ya taifa ya uganda, the cranes,yanaweza kuwa yamehitimisha historia ya kocha Mholanzi, Mart Nooij katika timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars baada ya kufungwa 3-0 na Uganda usiku huu katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza kufuzu michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) itakayofanyika Rwanda mwaka 2016, Sekisambu alimtungua kipa Deo Munishi ‘Dida’ bao moja kila kipindi, wakati bao la tatu lilifungwa na Farouk Miya dakika ya 89.

Mechi hiyo ni ya tano mfululizo Stars kufungwa, baada ya awali kufungwa na Madagascar, Lesotho, Botswana katika michuono ya COSAFA ambayo stars ilishiriki kama mwalikwa, na wiki iliyopita ikaambulia kipigo kutoka kwa misri.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni