Jumanne, 30 Juni 2015

MILLEN MAGESE, EDDY KENZO WAIBEBA EAST AFRICA TUZO ZA BET

tuzo aliotunukiwa Millen
Mwanamitindo na Mrembo wa Tanzania mwaka 2001, Happiness Millen Magese ametunukiwa tuzo ya pekee ya BET mwaka huu iitwayo ‘Global Good Award’
Millen amepewa tuzo hii kutokana na jitihada zake za kampeni ya ugonjwa wa endometriosis (ugonjwa unaosababishwa na seli za tumbo la uzazi kuwa nje ya kizazi) ambao amekuwa nao katika maisha yake yote tangu awe msichana.

Millen ameanzisha taasisi ya kuwasaidia wanawake wengine  hapa nchini ya Millen Magese Faundation ili waepuke kile ambacho kilimkuta yeye. Pamoja na hivyo Millen amekuwa mstari wa mbele kutoa misaada mbalimbali kwa wasiojiweza.

Eddy Kenzo kwenye red carpet akiwa na wapambe
Katika tuzo hizo pia msaani wa Uganda Eddy Kenzo amebeba tuzo ya msanii bora mpya wa kimataifa anayependwa na watazamaji (Viewer’s Choice Best New International Artist, 2015)
Kaitka kipengele hicho Eddy Kenzo alikuwa akichuana na Assper Nyovest wa Afrika kusini, Mz Vee wa Ghana na wasanii wa uingereza, George the poet, MIC Lowry Na Novelist

Kenzo katika ukurasa wake wa facebook amewashukru washabiki wake, huku akisema ilikuwa ni safari ndefu na akasema ni tuzo ya pekee kwa ukanda wa Afrika Mashariki.


Washindi wengine wa tuzo hizo ni kama ifuatavyo

 Breezy ameshinda tuzo ya Best Male R&B/Pop Artist na Fandemonium Awards, Beyonce aliondoka na tuzo za Best Female R&B/Pop Artist na Video of the Year kupitia video ya “7/11″. Nicki Minaj ameshinda Best Female Hip-Hop Artist na wimbo wake “Only” featuring Lil Wayne, Drake and Brown kushinda Coca-Cola Viewers’ Choice Award.
Muimbaji Janet Jackson alipokea tuzo ya kwanza ya Ultimate Icon: Music Dance Visual Award.
Upande wa Movie, waigizaji wa Empire Terrence Howard (Lucious) na Taraji P. Henson (Cookie) meshinda Best Actor na Best Actress.
Upande wa michezo Serena Williams ameshinda Sportswoman of the Year title. 
Hii ni orodha kamili ya washindi
• Ultimate Icon, Music Dance Visual Award: Janet Jackson
• Humanitarian Award: Tom Joyner
• Best New Artist: Sam Smith
• Best Female Hip-Hop Artist: Nicki Minaj
• Best Male Hip-Hop Artist: Kendrick Lamar
• Best Female R&B/Pop Artist: Beyonce Knowles
• Best Male R&B/Pop Artist: Chris Brown
• Best International Act UK: Stormzy
• Best International Act Africa: Stonebwoy
• Best Group: Rae Sremmurd
• Best Collaboration: Common & John Legend – “Glory”
• Best Actress: Taraji P. Henson
• Best Actor: Terrence Howard
• Youngstars Award: Mo’ne Davis
• Best Movie: “Selma”
• Best Gospel Artist: Lecrae
• Video of the Year: Beyonce Knowles – “7/11″
• Video Director of the Year: Beyonce Knowles, Ed Burke & Todd Tourso
• Sportswoman of the Year: Serena Williams
• Sportsman of the Year: Stephen Curry
• Coca-Cola Viewers’ Choice Award: Nicki Minaj Ft. Drake, Lil Wayne & Chris Brown – “Only”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni