Jumapili, 21 Juni 2015

KIBARUA CHA KOCHA NOOIJ CHAOTA NYASI TAIFA STARS

 kocha  wa stars aliyefungashiwa virago, Mart Nooij
Kibarua cha mholanzi Mart Nooij kimefikia tamati baada ya kikao cha  kamati ya utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kulichokaa  kujadili mwenendo wa timu ya taifa, Taifa Stars. Mkataba wa Nooij na Taifa Stars ulikuwa umebakia miezi 10

Pia Kamati hiyo imevunja  benchi la ufundi la timu hiyo mpaka benchi jipya litakapotangazwa.

Kibarua cha Nooij kinafikia tamati baada ya kufuingwa mechi tano mfululizo zikiwemo mechi kati ya Lesotho, Madagascar, Botswana, Misri na mechi ya jana dhidi ya Uganda ambayo Stars imeambulia kipigo cha mabao 3-0 katika uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Tangu Nooij aichukue stars April mwaka jana Kutoka kwa Kim Poulsen, ameiongoza timu hiyo katika mechi 18 kati ya hizo ameshinda mechi 3, sare mechi 6, na kufungwa mechi 9



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni