Kwa siku tatu mfululizo bunge limekuwa na mzozo ambao umekuwa ukipelekea kuahirishwa kwa vikao vya bunge huku, baadhi ya wabunge wakisimamishwa kuhudhuria vikao vilivyobaki vya bunge hilo ambalo linakoma July 8.
Alhamisi July 02 2015 Mbunge John Mnyika aliomba mwongozo kuomba Bunge lisiendelee kwa vile ishu ya kujadili Miswada mitatu iliyowasilishwa kwa hati ya dharura kwa siku moja ilikuwa inakiuka Kanuni za Bunge, ukatokea mvutano na baadae Spika Anne Makinda akaahirisha Bunge.
Ijumaa July 03 2015 hali ikawa hivyo hivyo tena, wakati Waziri George Simbachawene anasoma Muswada, ikatokea mvutano mwingine, zikaanzishwa kelele Bunge likaahirisha tena.. Kikao cha Jioni Spika Anne Makinda akarudi na list ya majina ya Wabunge ambao wamesimamishwa Bungeni kutokanana maamuzi ya Kamati ya Maadili ya Bunge.
Leo July 04 2015 Kikao kimeanza tena saa tatu asubuhi, Mbunge Ezekiel Wenjeakaomba Spika atoe ufafanuzi wa kwanini Mbunge Silinde hayuko kwenye list ya waliotajwa kusimamishwa lakini Askari wa Bunge wamemzuia asiingie kwenye Kikao?
Majibu ya Spika hayakuwaridhisha baadhi ya Wabunge, zikaanza tena kelele… Spika akataja list ya Wabunge wengine ambao wanasimamishwa kuhudhuria Vikao vya Bunge kwasiku tano kila mmoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni